Mahakama moja nchini Sweden imemhukumu mwanasoka wa ligi daraja la pili kwenda jela miaka 2 kwa kosa la kumbaka na kumpiga mkewe.
Baada ya kumaliza adhabu yake, Kwame Bonsu mwenye umri wa miaka 22, ambaye kabla ya kesi alikuwa akiitumikia klabu ya zamani ya mchezaji wa soka wa Tanzania Haruna Moshi Boban – Gefle IF Club, atafukuzwa katika nchi hiyo ya Scandanavia, ambapo amekuwa akiishi tangu miaka 4 iliyopita, mahakama ya Gavle District imeamua.
Klabu ya Gefle imesema Bonsu amefukuzwa kwenye klabu hiyo mara moja baada ya kupatikana na hatia ya mashtaka yake.
Mchezaji huyo pia ametakiwa kulipwa kiasi cha 245,000 kronor zaidi ya million 50 za kitanzania – ikiwa ni fidia kwa mkewe, ambaye ni raia wa Sweden.
Bonsu alikutana na mkewe mnamo mwaka 2014 wakati akiitumikia klabu ya Mjolby na wakaoana mwaka uliofuatia. Miezi kadhaa baada ya ndoa alisaini kwenda klabu ya Gafle – kilomita zaidi ya 300 kutoka Mjolby.
Post a Comment
Post a Comment