Uongozi wa mabingwa wa kihistoria Simba Sc imewasilisha rufaa Kwa Bodi ya ligi shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kudai pointi za mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Jumapili ya wiki iliyopita Kaitaba Bukoba na Simba kufungwa kwa magoli mawili kwa moja (2-1) na Kagera Sugar.
Katika Barua ya Simba imedai Kagera Sugar ilimtumia mchezaji Mohamed Fakhi mwenye kadi tatu za njano ambazo ni kukiuka kanuni na taratibu za ligi kuu ya Vodacom .
Kamati ya masaa 72 leo itakaa kupitia rufaa mbalimbali zilizowasilishwa kwenye kamati mojawapo ni hii rufaa ya Simba Kwa Kagera Sugar
Wakati haya yakifukuta uongozi wa Kagera Sugar umejitokeza na kukana rufaa hiyo, kocha wa Kagera sugar Mecky Maxime alisema: “Mimi niko makini sana na masuala ya kadi za wachezaji wangu, kila mchezaji wangu anapoonyeshwa kadi naandika na pia namkumbusha meneja wangu naye kuandika kadi, Simba kama wameshindwa kutafuta pointi uwanjani wasitafute sababu ya kupata pointi za mezani”
Pia Meneja wa kikosi hicho ambaye amesema Fakhi ana kadi mbili tu za njano na si tatu Kama wanavyosema
Post a Comment
Post a Comment