const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Kwa mara ya kwanza, bosi wa PSG azungumzia kuhusu taarifa za kumtaka Wenger - HABARI MPYA

..

Kwa mara ya kwanza, bosi wa PSG azungumzia kuhusu taarifa za kumtaka Wenger

Hali ya kocha Arsene Wenger pamoja na kuipandisha timu hiyo hadi nafasi ya tano lakini bado si nzuri, huenda siku za mwisho za Wenger zimekaribia hata isiwe ndani ya mwezi huu au ujao lakini mwisho umekaribia.

Tayari imeelezwa vilabu mbali mbali vimeanza kufuatilia sakata la Wenger na Arsenal kwa ukaribu zaidi. PSG, Real Madrid, Barcelona na baadhi ya timu za nchini China zimekuwa zikimtaka Mfaransa huyo.

Lakini PSG wamekuwa wakitajwa sana na kupewa nafasi kubwa kutoka na kwamba Wenger ni mzaliwa wa Ufaransa huenda angevutiwa na kurudi nyumbani kufundisha soka.

Sasa mkurugenzi wa PSG ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Barcelona Patrick Kluivert ameibuka na kuongelea suala hilo, Kluivert amesema habari hizo sio za kweli na zipuuzwe.

“Wenger kuja PSG?huo ni uongo na kuna asilimia sifuri ya hilo kutokea” alisema Kluivert, hiyo itakuwa imevunja minong’ono kuhush kocha huyo na PSG na sasa Real Madrid na Barcelona watakuwa ndio wanaoongelewa tu.

Keleleza kumpinga Wenger bado zinaendelea, japo ushindi wa bao 3 kwa 0 dhidi ya West Ham kidoogo.umeshusha presha kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Related Posts

Post a Comment