WINGA wa Yanga, Simon Msuva, amesema katika maisha yake ya soka hatasahau mwaka 2015 alivyozomewa na mashabiki wa klabu yake hiyo baada ya kukosa penalti dhidi ya Simba, ambapo walifunga bao 1-0 mpaka akajuta kuichezea timu hiyo lakini sasa mambo yako poa.
Msuva ambaye kwa sasa ana mabao 10 akiongoza kwenye msimamo wa wafungaji, alisema baada ya kukosa penalti hiyo mashabiki walishindwa kuvumilia wakaanza kumrushia maneno mazito huku wengine wakifikia hatua ya kumtaka aondoke.
“Maisha ya mpira wa miguu hasa unapochezea hizi timu mbili za Simba na Yanga yanataka uvumilivu sana, kwani bila hivyo unaweza ukaamua kuondoka kutokana na baadhi ya mashabiki kuwa na maneno makali.
“Nakumbuka msimu wa mwaka 2015 ilitokea penalti upande wetu nikachukua uamuzi wa kuipiga, lakini bahati mbaya sikufanikiwa kufunga nikatukanwa sana mpaka nikajua, mchezo huo ulimalizika kwa sisi kupoteza tukifungwa bao 1-0,” alisema.
Anasema tangu kukosa penalti hiyo alikosa raha kwani mashabiki walikuwa wakimzomea sana huku wengine wakiutaka uongozi kutomwongezea mkataba mpya, lakini hata hivyo alijipa moyo na yote hayo yakapita.
Jamaa atengeneza ndege YAFANIKIWA KURUKA
Post a Comment
Post a Comment