Arsenal imetambulisha ndege mpya ambayo itakuwa inaitumia kusafiria kwenda kwenye mechi zake za ugenini za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ndege hiyo ni ya kifahari na ina kila kitu kinachohitajika ndani. Klabu hiyo iliionyesha ndege hiyo kwenye Instagram wiki iliyopita, aina ya Emirates Airbus A380 nje ikiwa imepambwa na picha za mastaa watano wa timu hiyo; Hector Bellerin, Olivier Giroud, Santi Cazorla, Alexis Sanchez na Mesut Ozil.
Ndani ya ndege hiyo, kila mchezaji ana kitanda chake huku wakiwa wamewekewa anasa kibao, zikiwemo chaneli za televisheni 2,500 na kila mchezaji ana TV yake.
Ndani kuna baa ya kisasa yenye vinywaji vya kila aina, vyoo na mabafu lakini pia mazingira mazuri ya kukaa.
The Gunners wataipanda ndege hiyo kwa mara ya kwanza watakaposafiri kuifuata Bayern Munich mwezi ujao. Angalia picha.
Post a Comment
Post a Comment