const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Jinsi ya kufunga kompyuta yako kwa kutumia Flash drive - HABARI MPYA

..

Jinsi ya kufunga kompyuta yako kwa kutumia Flash drive

Itakuwaje kama flash tunazozitumia zikawa mbadala wa password tulizohifadhi kwenye vichwa vyetu? Hii inawezekana na program inayoitwa Predator. Leo nitakuonesha jinsi ya kutumia program hiyo kuifanya flash yako kuwa funguo ya kompyuta yako.

Funga kwa kutumia Predator

Hatua ya 1. Download software ya Predator hapa ambayo utaitumia kwenye kompyuta yako. Predator itakuwa kwenye format ya zip hivyo, fanya extraction halafu install.



Hatua ya 2. Kisha weka password pamoja na key ya dharula kwenye software hiyo.

Hatua ya 3. Unaweza weka password yoyote unayotaka, hakikisha umechagua flash drive sahihi ambayo itatumika kufungua kompyuta yako.

Hatua ya 4. Baada ya kuweka password flash yako itakuwa tayari kutumika. Unaweza ukaweka settings zingine mbali mbali kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Hivyo kila utakapo ingia kwenye kompyuta yako chomeka flash yako kisha fungua software hiyo fanya kazi zako ukimaliza ondoa flash. Kompyuta yako itajifunga na ili kuweza kuitumia tena itabidi uchomeke flashi hiyo tena ndipo itajifungua.

Funga kompyuta kwa kutumia Rohos USB Logon Key

Progam hii inatumia njia mbili za kuhakikisha ulinzi wa kompyuta yako ambapo inabadilisha flash yako kuwa kama funguo ya kufungulia kompyuta yako.

Hatua ya 1. Download hapa halafu fanyia installation Rohos Logon Key kwenye kompyuta yako kisha fungua software hiyo utaona screen kama hiyo hapo chini kwenye picha. Kisha bonyeza hapo walipo andika 'Setup USB Key.'



Hatua ya 2. Itakuja screen kama hiyo chini kwenye picha. chakufanya chagua 'USB Flash Drive' kwenye drop down menu ya pili.

Hatua ya 3. Kisha andika password unayotumia kwenye window yako halfu bonyeza kwenye 'Setup USB Key'.


Hatua ya 4. Kisha itakuletea message kama ilivyokwenye picha hapo chini 'Your USB Key has been successfully configured.'




Mpaka hapo nadhani utakuwa umefanikiwa kuweka password kwenye USB flash yako na utaweza kutumia USB flash hiyo kufungua kompyuta yako. Pia unaweza ukatumia software hiyo kufunga kompyuta zaidi ya moja natumai utakuwa umeipenda hii makala usisahau kutoa maoni yako hapo chini na kushare kwa rafiki zako.

Related Posts

Post a Comment