const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Snura alia na serikali kuhusu gharama ya kipimo cha DNA - HABARI MPYA

..

Snura alia na serikali kuhusu gharama ya kipimo cha DNA



Snura akiwa na binti yake

Msanii wa muziki na mama wa watoto wawili, Snura Mushi ameibuka na kuiomba Serikali iangalie uwezekano wa kupunguza gharama za kipimo cha vinasaba (DNA) ili watu wa hali ya chini waweze kumudu.
Akiongea na gazeti la Mwananchi, muimbaji huyo alidai kipimo hicho kikipatikana kwa urahisi, kitasaidia kupunguza kesi za wanaume kutelekeza watoto na kukataa mimba.

Nyota huyo alisema DNA ikiwa bei nafuu hata watu wasiokuwa na uwezo watamudu kupima tofauti na ilivyo sasa ambako wachache ndiyo hupima.

Sanjari na hilo, Snura alishauri itungwe sheria ambayo itambana mwanamume aliyempa mimba mwanamke na kukataa kulipia gharama za matunzo ya ujauzito.

“Ili kukomesha suala la kukataa mimba naona itungwe sheria ambayo itamlazimisha mwanamume kulipia gharama zote za matunzo endapo itakuja kuthibitika kisayansi kuwa mtoto ni wake. Kama anakataa mimba wala asilazimishwe asainishwe na mwanamke asubiri atakapojifungua ipimwe DNA, ikibainika kuwa mtoto ni wa mwanamume huyo atozwe gharama zote alizotumia mama kulea ujauzito,” alisema msanii huyo ambaye mwaka jana alifungiwa kutokana na video yake ya Chura kutozingatia maadili na sasa amejikita zaidi kwenye muziki wa Singeli.

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na video ya wimbo ‘Shindu’.

Related Posts

Post a Comment