const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Insta inayotumika kumtusi Diamond yaendelea kutoa matusi wakati mtuhumiwa mwenye akaunti yupo ndani - HABARI MPYA

..

Insta inayotumika kumtusi Diamond yaendelea kutoa matusi wakati mtuhumiwa mwenye akaunti yupo ndani



November 18, 2016 kijana mmoja ambaye jina lake halikutambulika mara moja alikamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kutumia akaunti ya ‘Shilolekiuno_official’ kuwatukana watu mbalimbali akimo Diamond pamoja na familia yake.

Kijana anayetuhumiwa kutukana watu kutumia akaunti ya Shilolekiuno_official akipelekwa segerea baada ya kukosa dhamana Disemba 13 2016 katika Mahakama ya Kinondoni

Lakini cha kushangaza akaunti hiyo bado inaendelea kumtukana watu wakati mtuhumiwa yupo ndani.

Sallam ambaye ni meneja wa Diamond ndiye aliyetoa taarifa za kukamatwa kwa kijana huyo mwezi Disemba mwaka jana.

“Kwa watu wote kama ulitukanwa na huyu ambae anaejiita @shilolekiuno_official kwa sasa yupo chini ya mikono ya sheria, Kama una mashitaka yoyote fika Oyster Bay Polisi, Vizuri ametaja watu wanaemtuma afanye hivyo! Na kuwasaidia wale ambao wanajiamini kuwa hawawezi kujulikana basi kwa taarifa yenu Serikali ina mkono mrefu sana! Eti Jana alikuwa anamuita Diamond “Simba” .” aliandika Sallam Insta baada ya kukamatwa kwa jina hiyo.

Hata hivyo kamanda wa polisi wa Kinondoni, Suzan Kaganda alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa hakuna kijana kama hiyo aliyekamatwa.

“Hatujamkamata na hatuna mtu kama huyo kituoni kwetu. Tuna vijana wengi ambao wamekamatwa wanamakosa kama hayo, jina kama hilo uliloniuliza halipo hapa kituoni kwetu labda kwenye kituo kingine.”

Hii ni baadhi kati ya post mpya za kwenye akaunti hiyo.

Related Posts

Post a Comment