const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); CHADEMA- Jengo la Makao Makuu ya Chama Ni Letu,Hakuna wa kutupa Notisi ya Kuhama..!! - HABARI MPYA

..

CHADEMA- Jengo la Makao Makuu ya Chama Ni Letu,Hakuna wa kutupa Notisi ya Kuhama..!!


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema nyumba iliyopo Mtaa wa Ufipa katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, inamilikiwa na chama hicho kupitia Baraza la Wadhamini.

Chadema imetoa ufafanuzi kutokana na taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa wamepewa notisi ya siku 14 na mmiliki wa jengo hilo, wanalotumia kama ofisi na Makao Makuu ya chama hicho, kuhama kutokana na kukiuka mkataba wa malipo na upangishwaji.

Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene akijibu uvumi huo, alisema chama hicho ni mmiliki halali wa jengo la Makao Makuu lililo chini ya Baraza la Wadhamini.

“Kama kuna mmiliki wa jengo hilo ajitokeze, lakini nawahakikishia hakuna hivyo puuzeni habari zinazozagaa,” alisema Makene na kuongeza kuwa kuna hati ya jengo hilo, iliyoandikwa mmiliki wa jengo hilo ni Chadema. Alisisitiza watu wapuuzie propaganda hizo, zinazopanga kuwahadaa wanachama na Watanzania kwa ujumla.

Related Posts

Post a Comment