Haya ndio madhara ya kufanya mapenzi kupita kiasi. Soma Hapa



Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono.



Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.

Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari, hapa nimeweka chumvi kidogo lakini huo ndio ukweli halisi.

Twende pamoja katika kutazama madhara hayo kwa kina.

1 . Kupoteza hamu ya tendo la ndoa.

Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara.

Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.

2 .Kuujaza mwili tamaa kubwa.

Tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi na kwa wakati gani?

3 .Kupoteza raha kamili ya tendo.

Raha ya tendo hutegemea sana hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na kiu ya kufanya mapenzi, hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo haikutoshi kumaliza tamaa yako. Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo!

4. Kupoteza nguvu ya mwili.

Madhara mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili.

5 .Kupatwa na magonjwa.

Kama tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa na tamaa na hujikuta wanafanya mapenzi holela ambayo huweza kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.

Related Posts

Post a Comment