Diamond afunguka kuwa hana tatizo na baba yake, Asema penye kumsaidia anafanya hivyo

Msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameweka wazi kuwa kwa sasa hana tofauti yoyote na baba yake mzazi (Mzee Abdul) kwamba wanaongea na kwamba anapohitajika kusaidia anafanya hivyo.

Hayo Diamond ameyasema leo alipokwenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya suluhisho la shauri lake na mzazi mwenzie, Hamisa Mobetto.

“Nyuma yanyuma ya stori hii nimejifunza kuwa si kila mtoto ambaye haishi na mama au baba basi hasiyeishi nae ana matatizo… hata hii imenifunza kwa mama na baba yangu sometime naweza nikawa nammaindi kumbe kina vitu vingine ambavyo wazazi wetu walivifanya vinakuwa sio fresh.

“Kama mtoto angeweza kukua hajua nyuma angeweza kusema ‘Dingi’ noma kweli kumbe ni majivuno tu ya watu wawili kwahiyo wazazi watumie busara kisuruhisha matatizo yao ili yasiwaumize watoto.

“Sasa hivi niko freshi tu na baba yangu nawasiliana naye penye kusaidia nasaidia nikiwa sina uwezo namwambia lakini kwa bahati mbaaya haatukuweza kuwa na mahusiano ya karibu kama ilivyo kwa mama kwasababu hatukusoeana sana.

“Kuna vitu vingine una kuwa na woga wa kumwambia mfano ninavyomwambia mama twende sehemu fulani unakuwa na woga nikimwambia atanifikiriaje kwahiyo watu kutoniona nipo naye kwenye hadhara wanajua Diamond hayuko poa na baba yake sio kweli. amesema

Related Posts

Post a Comment