Mkoa wa Njombe umeanza kuandaa timu ya watoto wenye Ulemavu
wa akili na wenye usonji itayo uwakilisha mkoa huo katika mashindano ya kitaifa
yanayotarajiwa kufanyika Zanzibar Mwezi Decemba mwaka huu .
Katika kuhakikisha kikosi kitakachopatikana kinauwakilisha
mkoa vyema na kurejea nyumbani na medali za kutosha ,tayari kumeanza kufanyika
mchakato wa kusaka vipaji vya kundi hilo maalumu la watoto wenye ulemavu
kuanzia ngazi ya halmashauri ambako mchujo mkali utafanyika ili kupata timu
yenye wachezaji 15 ambao wata ambatana na watu 3 wa benchi la ufundi kwenda
Zanzibar.
Akizungumzia maandalizi hayo mratibu wa Special Olimpics Mkoa
wa Njombe Happy Mpete anasema pamoja na mkoa kujikita katika kuandaa timu yenye
wachezaji 15 itakaoshiriki mashindano ya
Special Olimpics mwezi dec Kisiwani Zanzibar kwa watoto wenye umri wa
miaka 2 hadi 7 , pia mkoa umeanza kuandaa timu nyingine ya watoto walemavu
wenye kuanzia miaka 8 na kuendelea.
Amesema lengo la serikali na mashirika mengine ya haki za
binadamu kuanzisha michezo ya watu wenye ulemavu hususani viziwi, mabubu
,vichwa vikubwa na michezo mingine ni kutokomoza imani mbaya dhidi ya watu
wenye mahitaji maalumu .
Happy Mdende na
Maltina Ngatunga ni miongoni mwazazi ambao wameguswa na kushawishika kupeleka
watoto wao kujiunga na mazoezi ya kusaka kikosi cha watoto walemavu wa akili na
wenye usonji kitakachouwakilisha mkoa katika mashindano hayo Zanzibar na
kueleza jinsi mazoezi hayo yanavyohimalisha viungo vya watoto wao.
Michezo itakayoshindaniwa katika mashindano hayo ni pamoja
na Riadha , Kuruka Kamba, Mpira wa pete na Mpira wa miguu ambapo hadi sasa watoto
30 wamesajiliwa na kushuhudia wakianza mazoezi kwa furaha zote
Post a Comment
Post a Comment