TzTown Tv: Tazama watoto wakieleza kilicho wapata baada ya kuzimia na nini kimesababisha wazimie

Post a Comment
WAZAZI wa watoto wa shule ya Msingi Igola Halamashauri ya Mji Njombe wilayani na mkoa wa Njombe wamelalamikiwa kuwashawishi na kuwanyesha dawa watoto wao kuanguka kanakwamba wanamapepo ili kupata fidia ya maeneo ambapo imejengwa shule hiyo.
Hayo yanabainishwa na mwalimu mkuu wa shule ya Igola baada ya watoto hao kuanguka mara kwa mara kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu ambapo inabainika baada ya Afisa elimu kuwatisha watoto hao na kuweka wazi.
Wakazi wa kijiji Igola eneo ilipo shule hiyo wanasema kuwa ni baadhi yao ambao wanafanya vitendo hivyo kwa madai ya kudai eneo ambalo walilito kwaajili ya kujenga shule hiyo.
Wanafunzi wanaeleza kile ambacho huwa wamekuwa wakikishuhudia shuleni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Njombe akizungumza na wakazi wa kijiji hicho anapiga marufuki vitendo hivyo.

Tazama watoto wakieleza kilicho wapata baada ya kuzimia na nini kimesababishwa wazimie............

Related Posts

Post a Comment