TzTown Tv: Marufuku kuharibu misitu ya asili

Post a Comment
Serikali wilayani Njombe imepiga marufuku uharibifu wa misitu ya asili pamoja na vyanzo vya maji kutokana na kuwepo kwa baadhi ya wananchi wanaofanya shughuli za kilimo katikati ya misitu mikubwa na kusababisha uharibifu mkubwa wa ikolojia.
Mkuu wa wilaya ya njombe akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake anasema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya iko tayari kuinusuru misitu wilayani humo iliyoko kwenye hifadhi na hakuna mtu anayeruhusiwa kuendeleza uharibifu.
Anasema kwa waliokwisha fanya kilimo ifikapo msimu wa Mavuno hapo septemba mwaka huu wanatakiwa kuacha mara moja kuendeleza kilimo ndani ya misitu na maagizo yamewasilishwa katika serikali za vijiji ili kuweka mipaka ya misitu.
Lakini kuna uhimu gani kuitunza misitu ya asili mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya njombe valentine hongoli anafafanua.

TAZAMA VIDEO MISITU NYUMBE YAVAMIWA..........

Related Posts

Post a Comment