Mohamed Thabalala wa Simba Anyakua Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligu Kuu Msimu wa 2016/17..!!!

Beki wa kushoto wa kutumainiwa wa klabu ya Simba, Mohamed Hussein Hussein 'Tshabalala' a.k.a Zimbwe Jr. amefanikiwa kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliomalizika wa 2016/17.
Zimbwe amewashinda Aishi MANULA (Azam) na Saimon MSUVA (Yanga na ameondoka na kitita cha shilingi milioni 10.

Beki huyo ambaye amecheza michezo yote ya Simba ya ligi kuu msimu huu kwa dakika zote 90 kwa kila mchezo ametangazwa rasmi katika sherehe zilizofanyika usiku wa jana Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Mbali na tuzo hiyo ambayo ndiyo kubwa, tuzo nyingine zilizotolewa ni kama ifuatavyo... 
Tuzo ya Goli Bora la Msimu inakwenda kwa Shiza Kichuya, bao alilofunga Feb. 25 katika mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga. Kichuya, amewashinda Peter Mwarianzi na Zahoro Pazi

Tuzo ya Heshima inakwenda kwa Kitwana Manara mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars aliyewika miaka ya 1960 hadi 1970

Tuzo ya Ismail Khalfan (U-20) inakwenda kwa Shaaban IDD (Azam) akiwashinda Abdalah MASOUD (Azam) na Mosses KITAMBI (Simba)

Mchezaji Bora Chipukizi ni Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar), akiwashinda Shaaban IDD (Azam) Mohammed ISSA (Mtibwa)

Mchezaji Bora wa Kigeni ni Haruna NIYONZIMA (Yanga), akiwashinda Method MWANJALE (Simba) na Yusuph NDIKUMANA (Mbao FC)

Tuzo ya Kipa Bora imekwenda kwa Aishi MANULA (Azam) akiwashinda Owen CHAIMA (Mbeya City) na Juma KASEJA (Kagera Sugar)

Tuzo ya Kocha Bora imekwenda kwa Mecky MEXIME (Kagera Sugar) akiwashinda Joseph OMOG (Simba) na Ettiene NDAYIRAGIJE (Mbao FC)

Tuzo ya mwamuzi bora imekwenda kwa Elly SASII (DSM) miaka 29, amewashinda Shomari LAWI (Kigoma) na Hance MABENA

Tuzo ya mfungaji bora imekwenda kwa Saimon Msuva (Yanga) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting), zawadi yao ni Tsh. mil 5.8

KIKOSI BORA (4:4:2): Manula (Azam), Kimenya (Prisons), Tshabalala (Simba), Yakub (Azam), Mwanjale (Simba), Kenny Ally (Mbeya City), Msuva (Yanga), Niyonzima (Yanga), Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting), Mbaraka (Kagera Sugar), Kichuya (Simba)

Related Posts

Post a Comment