MAMBO 5 YANAYOWAFELISHA BLOGGER'S WA BONGO

Habari karibu tena tupeane mawili matatu katika haya tunayapenda kama kawaida Riyadi Bhai Napenda kukupa dondoo na maarifa tofauti tofauti 

tuangalie Baadhi ya makosa yanayowafelisha bloggers wengi hapa bongo, katika tafiti zangu nimegundua baadhi ya mambo yanayowakwamisha blogger wengi hapa nchini.
Kuiga
jambo la kwanza linalowakwambisha blogger wengi ni kufuata mkumbo yaani mtu akisikia kuwa blog inalipa yeye hana haja ya kujua njia zipi zinazofanya blog kuitwa inalipa yeye uamua tu kufungua blog ilamradi tu amesikia blog inalipa

kukosa mada za kuweka
blogger wengi hushindwa kuendesha blog zao kwa kukosa mada za kuandika uishia kukopi na kupesti kutoka katika blog kubwa mwisho wa wanashindwa kuendelea kutokana na kukosa watembeleaji wa uhakika.

Uvumilivu/Subra
wengi katika blogger wanafeli kutokana na kukosa uvumilivu, kwakweli kubloging kunahitaji uvumilivu wa hali ya juu sio kublogging pekee ispokuwa kila jambo linahitaji subira ili kufanikiwa katika jambo hilo.

Kukosa vitendea kazi
blogger wengi hapa nchini hawana vitendea kazi kama laptop,camera n.k hivyo kunawafanya kukosa ufanisi katika kazi yao ya bloging, wanategemea zaidi internet cafe jambo ambalo linawafanya kukosa kuwa na uhuru na kitu wanachokifanya, sababu kama unahusiki na blog ya habari huwezi kuweka habari za hizi punde kama zitakuwa zimetokea usiku mnene.

Kukosa sapoti
familia zetu nyingi hazinaufahamu kuhusu biashara ya online, hivyo inapelekea kukosa sapoti kuhusu jambo lako unalolifanya, kuna wakati sisi kama binanamu tunahitaji msaada japo wa mawazo kutoka kwa watu wetu wa karibu lakini tunakusa msaada huo na kutupelekea kuvunjika moyo.

Haya ni mawazo yangu kutokana na mambo niliyokumbana nayo kwangu na kwa watu wangu wa karibu, unaweza kuniachia maoni yako hapo chini kuhusu changamoto unazokutana nazo.

Related Posts

Post a Comment