Hivi Ndivyo Taifa Linavyoibiwa Madini Mchana Kweupee..!!!

Kamati iliyoundwa na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kuchunguza mchanga wenye madini aliokuwa ameuzuia kusafirishwa nje ya nchi, hii ljana imewasilisha taarifa ya uchunguzi ilioufanya ikiwa na mambo 8 pamoja na mapendekezo 9.

Kamati hiyo imebaini mambo makuu 8 kama ifuatavyo......

1. Dhahabu

Kamati imebaini kuwepo kwa viwango vingi vya juu vya dhahabu ndani ya makinikia yaliyofanyiwa uchunguzi. Viwango hivyo ni kati ya 671 g/t hadi 2375 g/t, sawa na wastani wa 1400 g/t. Wastani huu ni sawa na 28 kg za dhababu kwenye kontena moja lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kwenye makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na wastani wa tani 7.8 za dhahabu yenye thamani ya TZS bilioni 676 (USD 307,292,720).

Aidha, kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwenye kontena moja lenye shehena ya tani 20 za makinikia (47.5 kg), kiasi cha dhahabu katika makontena 277 kitakuwa 13,157.5 kg ambazo thamani yake ni TZS 1,146,860,330,000 (USD 521,300,150).

Hivyo, thamani ya dhahabu katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147.

Taarifa tulizopata kutoka kwa wazalishaji pamoja na Wakala wa Serikali wa Ukaguzi Madini (TMAA) zinaonesha kuwa makinikia yana wastani wa takriban 200 g/t. Kiwango hiki ni sawa na kilo 4 za dhababu kwenye kila kontena. Hivyo, makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na tani 1.1 za dhahabu. Kiasi hiki cha dhahabu kina thamami ya TZS bilioni 97.5 (USD 44,320,000).

Thamani hii ni ndogo sana ukilinganisha na thamani halisi iliyopatikana katika uchunguzi huu ya kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147. Kutokana na tofauti hii kubwa kati ya viwango vya dhahabu vilivyopo kwenye taarifa za usafirishaji na vile ambavyo Kamati imevibaini, ni dhahiri kuwa Taifa linaibiwa sana kupitia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi.

2. Pamoja na viwango vikubwa vya dhahabu kwenye makinikia, Kamati ilipima na kupata viwango vikubwa vya madini ya copper (kiwango cha 15.09% hadi 33.78%, wastani wa 26%), silver (kiwango cha 202.7 g/t hadi 351 g/t, wastani wa 305 g/t), sulfur (kiwango cha 16.7% hadi 50.8%, wastani wa 39.0%) na iron (kiwango cha 13.6% hadi 30.6%,wastani wa 27%).

Copper

Wastani wa kiwango cha copper kilichopatikana ni tani 5.2 na kiwango cha juu kilichopimwa ni tani 6.75 kwenye kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kiasi cha wastani wa copper kwenye makontena 277 ni tani 1,440.4 ambazo thamani yake ni TZS bilioni 17.9 (USD 8,138,260) na kiasi cha juu ni tani 1,871.4 ambazo zina thamani ya TZS bilioni 23.3 (USD 10,573,478). Hivyo, thamani ya copper katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 17.9 na bilioni 23.3.

Related Posts

Post a Comment